Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 05:32

UN yasema ghasia zaongezeka Myanmar


 Michelle Bachelet
Michelle Bachelet

Kamshina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ijumaa amesema ghasia nchini Myanmar zimeongezeka.

Pia amesema hali hiyo inazidisha mzozo ulioanza wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya Februari 1, ambayo yaliiangusha serikali iliyochaguliwa kidemokrasias ya Aung San Suu Kyi.

Michelle Bachelet amesema katika taarifa mjini Geneva, “kwa zaidi ya miezi minne tu, Myanmar imetoka kuwa demokrasia dhaifu na kuwa janga la haki za binadamu.”

Bachelet ameutupia lawama uongozi wa kijeshi wa Myanmar akisema ulihusika peke yake kwa mzozo huo na lazima uwajibishwe.

Afisi ya Bachelet anasema kuna ripoti za kuaminika kwamba watu 860 waliuawa na wanajeshi tangu Februari 1, na zaidi ya watu 4,800 wakiwemo, wapinzani wa utawala wa kijeshi, wanaharakati wa mashirika ya kiraia na wanahabari, wamewekwa kizuizini kiholela.

Chanzo cha Habari : VOA News

XS
SM
MD
LG