Onyo hilo limetolewa baada ya mashambulizi mabaya ya kijeshi yaliyo wafanya maelfu ya watu kukimbia makazi yao katika jimbo la Kayah.
Katika taarifa ya Jumatano, Tom Andrews mwakilishi maalumu wa UN Myanmar ametaka mwitikio wa haraka wa kimataifa.
Ameongeza kusema mashambulizi ya kijeshi ambayo yameshamiri baada ya mapinduzi ya Febuari, yanaendelea kutishia maisha ya maelfu ya watu wakiwemo wanawake na watoto katika majimbo ya Kayah ama Karenni.
Mwito huo umetolewa saa kadhaa baada ya ofisi ya UN ya Myanmar kueleza kwamba watu takriban 100,000 kukosa makazi mjini Kayah.
Chanzo cha Habari : Shirika la Habari la AP