Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:56

UN yaeleza jeshi la Myanmar lilivyosababisha janga la wakimbizi


Tom Andrews
Tom Andrews

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Myanmar, Tom Andrews anasema juhudi za jeshi la Myanmar za kuzima malalamiko dhidi ya mapinduzi zimesababisha karibu wakazi  250,000 kukimbia makazi yao.

Na wakati huo huo wanaharakati katika nchi hiyo ya Asia ya Kusini wanaendelea na maandamano ya kutaka kuachiliwa kwa watu waliokamatwa tangu mapinduzi ya Februari mosi.

Waandanamaji wakipinga mapinduzi ya kijeshi huku wamebeba picha za kiongozi aliyepinduliwa Aung San Suu Kyi mjini Kamayut, Yangon, Myanmar Alhamisi April 8, 2021.
Waandanamaji wakipinga mapinduzi ya kijeshi huku wamebeba picha za kiongozi aliyepinduliwa Aung San Suu Kyi mjini Kamayut, Yangon, Myanmar Alhamisi April 8, 2021.

Andrews kwa mara nyingine tena Jumatano ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za kimataifa akisema ameshtushwa sana kusikia kutoka duru anazozifahamu mashambulio ya wanajeshi yamewasababisha wakazi robo milioni wa Myanmar kuhama makazi yao.

Wito huo ulitolewa wakati nchi jirani na Myanmar zikijitayarisha kwa mkutano wa viongozi mjini Jakartra, Indonesia siku ya Jumamosi ili kulijadili suala hilo la mapinduzi.

Wanachama 10 wa Jumuia ya Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia, ASEAN, wamekuwa wakijaribyu kuishuari nchi hiyo mwanachama, juu ya namna ya kusitisha umwagikaji damu uliotokana na mapinduzi.

Bendera za nchi wanachama wa Jumuiya ya ASEAN
Bendera za nchi wanachama wa Jumuiya ya ASEAN

Lakini kutokana na kanuni za jumuia hiyo ya kupatikana maridhiano katika suala lolote lile na kutoingilia kati mambo ya ndani ya nchi mwanachama kumezuia uwezo wake kutanzua maoni yanayo tofuatiana juu ya namna ya kukabiliana na mauaji ya mamia ya watu yaliyofanywa na wanajeshi.

XS
SM
MD
LG