Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:59

Jeshi la Myanmar lamfungulia Suu Kyi mashtaka sita


Waandamanji wakipinga mapinduzi wakipita sokoni na picha za kiongoz aliyepinduliwa Aung San Suu Kyi katika mji wa Kamayut, Yangon, Myanmar Alhamisi, April 8, 2021.
Waandamanji wakipinga mapinduzi wakipita sokoni na picha za kiongoz aliyepinduliwa Aung San Suu Kyi katika mji wa Kamayut, Yangon, Myanmar Alhamisi, April 8, 2021.

Utawala wa kijeshi huko Myanmar umefungua shtaka la sita dhidi ya kiongozi wa kiraia aliyeondolewa madarakani, Aung San Suu Kyi, siku ya Jumatatu.

Wakati mashtaka hayo yanafunguliwa maandamano yamekuwa yakiendelea dhidi ya mapinduzi ya Februari 1.

Min Min Soe, wakili wa Suu Kyi, aliwaambia waandishi wa Habari kwamba mteja wake alishtakiwa kwa mara ya pili kwa kukiuka kanuni za nchi hiyo za COVID-19, wakati akionekana mahakamani kupitia njia ya video.

Min Min Soe anasema Suu Kyi aliiomba mahakama imruhusu kukutana na mawakili wake ana kwa ana wakati wa kikao cha Jumatatu.

Suu Kyi mwenye umri wa miaka 75, tayari anakabiliwa na mashtaka ikiwemo kuwa na redio sita za mkononi, shtaka kubwa zaidi la kuvunja sheria za siri za enzi za ukoloni, ambalo linaweza kumweka gerezani kwa miaka 14 akikutwa na hatia.

XS
SM
MD
LG