Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:12

Jeshi Myanmar ladaiwa kufanya mauaji zaidi


Waandamanaji wakijificha wakati wa maandamano ya kupinga mapinduzi ya kijeshi mjini Mandalay, Myanmar Machi 15, 2021. REUTERS/Stringer
Waandamanaji wakijificha wakati wa maandamano ya kupinga mapinduzi ya kijeshi mjini Mandalay, Myanmar Machi 15, 2021. REUTERS/Stringer

Mamlaka nchini Myanmar imeongeza sheria za kijeshi katika maeneo zaidi ya jiji kuu la Yangon Jumatatu huku kukiwa na ripoti za mauaji zaidi ya waandamanaji mikononi mwa vikosi vya usalama.

Kituo cha habari cha MRTV kinachoendeshwa na serikali kilitangaza kuwa wilaya za Dagon Kaskazini na Kusini, Dagon Seikkan na Okkalapa Kaskazini ziko chini ya sheria za kijeshi, siku moja baada ya vikosi vya usalama kuua watu wasiopungua 40 kote nchini Myanmar.

Mauaji mengi yalitokea katika kitongoji cha Yangon huko Hlaingthaya, na kuifanya kuwa siku ya umwagaji damu zaidi ya maandamano dhidi ya utawala wa kijeshi ambao ulichukua madaraka katika mapinduzi ya Februari mosi.

Mamlaka iliweka sheria ya kijeshi kwa Hlaingthaya, kitongoji cha jiji kuu la Myanmar, baada ya viwanda kadhaa vinavyomilikiwa na Wachina kuchomwa moto na karibu watu 2,000 kuzuia magari ya zima moto kuwafikia, kulingana na shirika la habari la Reuters likikariri televisheni inayoendeshwa na jeshi la Myawaddy. China inaonekana kuunga mkono utawala wa kijeshi wa Myanmar.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Zhao Lijian alitoa majibu juu ya shambulio la Jumapili kwenye viwanda hivyo wakati wa mkutano na wanahabari leo akisema kuchomwa na uporaji wa viwanda vya China ni chuki tunatumai kuwa upande wa Myanmar utachukua hatua madhubuti kulinda usalama wa raia wa China nchini Myanmar.

XS
SM
MD
LG