Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:23

Marekani yaweka vikwazo zaidi kwa maafisa Myanmar


Marekani jana imetangaza vikwazo dhidi ya maafisa wengine wawili wa Myanmar na kampuni mbili zenye uhusiano na jeshi la Myanmar.

Katika taarifa ya wizara ya fedha, Marekani inasema vikwazo hivyo ni matokeo ya kampeni ya serekali inayoendelea ya manyanyaso na vitisho dhidi ya waandamanaji wa amani na mashirika ya kiraia.

Hakuna maelezo ya mara moja kutoka serekali ya Myanmar.

Jeshi lilichukua madaraka tarehe 1 Februari katika mapinduzi, na kuiondoa serekali ya kiraia na kumzuia kiongozi wa nchi Aung San Suu Kyi na maafisa wengine wa ngazi ya juu.

Mmoja ya waliochukuliwa vikwazo ni Than Hlaing, kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya fedha, aliteuliwa kama mkuu wa jeshi la polisi na naibu waziri wa mambo ya ndani tarehe 2 Februari.

Mwingine aliyechukuliwa vikwazo ni Luteni jenerali Aung Soe, ambae wizara ya fedha inasema ni kamanda wa idara ya operesheni maalumu na anaripoti moja kwa moja kwa kiongozi wa kijeshi wa Myanmar Jenerali Min Aung Hlaing.

Waliochukuliwa vikwazo, mali wanazomiliki kwa asilimia 50 au zaidi ambazo ziko marekani na kuwa mikononi au kudhibitiwa na raia wa marekani zitazuiwiliwa.

Na umoja wa ulaya pia umetoa taarifa ya kuzuia mali za kiongozi wa kijeshi Min Aung Hlaing na marufuku ya kutopewa visa yeye na maafisa wa ngazi ya juu katika jeshi Pamoja na kiongozi wa tume ya taifa ya uchaguzi.

XS
SM
MD
LG