Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:18

Bunge la Israeli latarajiwa kuidhinisha uundaji wa serikali mpya


Naftali Bennett (L) akiwa na Yair Lapid
Naftali Bennett (L) akiwa na Yair Lapid

Bunge la Israel Jumapili linatarajiwa kuidhinisha uundaji wa serikali mpya na kumaliza utawala wa miaka 12 wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Serikali inayotarajiwa imeundwa na ushirika wa vyama ambapo ina wingi mdogo wa kiti kimoja katika bunge.

Hii pia itamaliza zaidi ya miaka miwili ya mkwamo wa kisaisa ambapo chaguzi tatu zilipelekea kutokamilika inavyotakiwa.

Naftali Bennet mzalendo wa mrengo wa kulia anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu katika makubaliano ya kushirikiana madaraka na kiongozi mwenye msimamo wa mrengo wa kati.

Kwa mujibu wa makubaliano ya ushirika, Bennet ambaye anaongoza chama cha Yamina, atashikilia madaraka mpaka September 2023, wakati atakapokabidhi kwa Yair Lapid kiongozi wa Yesh Atid, kwa miaka mingine miwili.

Netanyahu, aliyeshikilia wadhifa huo kwa muda nchini Israel, ambaye ametawala uwanja wa kisiasa kwa miaka mingi , atabakia kuwa mkuu wa chama cha mrengo wa kulia cha Likud na kuwa kiongozi wa upinzani.

Chanzo cha Habari : Reuters

XS
SM
MD
LG