Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:09

Makubaliano ya vyama Israeli yapokewa kwa hisia mchanganyiko


Kiongozi wa chama cha Kiislam cha Waarab Waisraeli Raam Raam Mansour Abbas (Kulia) akisaini makubaliano ya kuungana na kiongozi wa upinzani wa Israeli Yair Lapid (Kushoto) na milionea wa mzalendo wa mrengo wa kulia Naftali Bennett huko Ramat Gan karibu na mji wa pwani ya Tel Aviv
Kiongozi wa chama cha Kiislam cha Waarab Waisraeli Raam Raam Mansour Abbas (Kulia) akisaini makubaliano ya kuungana na kiongozi wa upinzani wa Israeli Yair Lapid (Kushoto) na milionea wa mzalendo wa mrengo wa kulia Naftali Bennett huko Ramat Gan karibu na mji wa pwani ya Tel Aviv

Waisraeli wanatoa hisia zinazo tofautiana kutokana na habari za kufikiwa makubaliano ya kuundwa kwa serikali ya mseto ya vyama vyenye itikadi tofauti.

Kuna baadhi wanaofurahia, wengine wakiwa na wasiwasi serikali ya mungano haitodumu na waarabu wakihisi hakuna kitakachobadilika.

Maoni ya ujumla ya Waisraeli wengi yanaeleza furaha na kuridhika kwamba huenda hawatalazimika kushiriki kwenye uchaguzi wa tano katika muda wa karibu miaka miwili baada ya makubaliano ya kihistoria yaliyotangazwa Jumatano.

Mkazi wa Tel Aviv

Chen Kostukovsky mkazi wa Tel Aviv anasema huu ni wakati wa kihistoria na habari nzuri baada ya kipindi cha Corona.

Kostukovsky anaeleza : "Tuna furaha sana kwa sababu baada ya miaka miwili migumu hatimae tumepata serikali. Tumesherehkea baada ya kufahamu kamba Lapid na wanasiasa wengine wamefikia makubaliano."

Makubaliano hayo yalitangazwa jana usiku na kiongozi wa upinzani Yari Lapid baada ya kumuarifu rais Reuven Rivlin kwamba amefanikiwa kuunda serikali ya muungano itakayoweza kufikisha kikomo utawala wa muda mrefu kabisa wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Muungano huo una wabunge 61 wanaohitajika kuidhinisha serikali hiyo katika siku zijazo katika bunge la Knesset. Chama kilichowezesha makubaliano hayo kufikiwa ni chama kidogo cha Kiislamu cha Waarabu Raam, baada ya kiongozi wake Mansour Abbas kukubali kuungana na vyama vya mrengo wa kulia ili kuweza kumuondoa Netanyauhu.

Kiislamu cha Waarabu Waisraeli

Mansour Abbas Kiongozi wa chama cha Raam anaeleza : "Nimetia saini makubaliano na Yair Lapid ili tuweze kuunda serikali baada ya kufikia makubaliano nyeti juu ya masuala yatakayosaidia maslahi ya Waarabu."

Serikali hiyo mpya inachanganya pamoja vyama vya siasa kali vya mrengo wa kulia, na vile vya siasa za kati, na siasa na kushoto hadi siasa kali za kushoto.

Kutokana na hayo Netanyahu hii leo kwenye ujumbe wa Twitter kwa mara nyingine amejitokeza kupinga muungano akitoa wito kwa vyama vyote vya mrengo wa kulia vilivyochaguliwa na wananchi kutokubali kuungana na serikali hiyo anayosema ni ya mrengo wa kulia itakayo hatarisha usalama wa Israeli.

Waisraeli Wenye Wasiwasi

Kwa Israeli wenye wasiwasi wanahisi huu ni mchanganyiko ambao hauwezi kufanyakazi pamoja.

Daphna Liel mwandishi wa masuala ya kisiasa wa kituo cha Chanel 12 ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba kuna mambo yasiyofahamika.

Liel anaeleza : "Tangazo la Lapid linababaisha. Israel haingi bado katika enzi mpya. Kungali na mvutano wa kisiasa. Hata kama Lapid na Bennett watafanikiwa kuunda serikali itakua dhaifu na wakishindwa Netanyahu anarudi."

Lapid alifanikiwa pia kufikia makubaliano kutokana na kuungwa mkono na kiongozi wa siasa kali za mrengo wa kulia, mshirika wa zamani wa Netanyahu, Naftali Bennett.

Kulingana na makubaliano yao, Bennette atakuwa Waziri Mkuu kwa miaka miwili na kumkabidhi madaraka Lapid miaka miwili ilyobaki katika muhula wao wa miaka minne. Bunge linabidi kukutana kumchagua spika kwanza kabla ya kupiga kura kuidhnsha serikali mpya.

XS
SM
MD
LG