Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:30

Mwaafaka wa upinzani waweza kumuondoa Netanyahu madarakani


Naftali Bennett (kushoto) akizungumza na Yair Lapid
Naftali Bennett (kushoto) akizungumza na Yair Lapid

Vyama vyenye mirengo tofauti ya kisiasa nchini Israel vimefikia mwaafaka Jumatano ambao unaweza kumuondoa Waziri Mkuu wa muda mrefu Benjamin Netanyahu kwenye wadhifa wake.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu

Kiongozi wa chama cha Yesh Atid, Yair Lapid amesema Jumatano dakika chache kabla ya muda wa mwisho wa kufikia makubaliano kukamilika amepata uungwaji mkono.

Muda huo ulikuwa usiku wa manane majira ya Israel akieleza alipata uungwaji mkono wa vyama vyenye wabunge wengi kwenye bunge la Knesset.

Lapid aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook akiahidi kwamba serikali itakayoundwa itawatumikia wananchi wote wa Israeli.

Naftali Bennett ambaye anaongoza chama cha mrengo mkali wa kihafidhina, Yamina party, alitangaza Jumapili kuunga mkono muungano wa Lapid.

Kulingana na makubaliano kati ya Lapid na Bennet, Bennet atahudumu kama Waziri Mkuu kwa kipindi cha miaka miwili, baadaye amuachie nafasi hiyo Lapid.

XS
SM
MD
LG