Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Gabi Ashkenazi amekutana na waziri mwenzake wa Misri Sameh Shoukray mjini Cairo.
Pia mkuu wa idara ya ujasusi wa Misri Abbas Kamel amekutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Jerusalem, kuzungumzia juu ya kuimarisha makubaliano ya kusitisha mapigano pamoja na kuimarisha ushirikaino kati ya nchi hizo mbili.
Kemal alikutana pia na Rais Mahamoud Abass mjini Ramallah kwa mazungumzo kama hayo.
Wachambuzi wanasema Wapalestina kwa muda mrefu wamekuwa wamegawika kati ya Hamas na Fatah lakini mapigano ya hivi karibuni kati ya Israel na Hamas yameweza kuunganisha pande hizo mbili za Wapalestina katika njia ambayo haijawahi kushuhudiwa kwa miaka mingi.