Uamuzi huu unatokana na kuendelea kwa janga la virusi vya corona.
Tangazo lilitolewa na ufalme huo linakuja baada ya hatua kama hiyo kuchukuliwa mwaka 2020 kuhusu Ibada ya Hijja kutokana na virusi, lakini bado iliruhusu idadi ndogo ya waumini kushiriki katika ibada hiyo.
Taarifa iliyotangazwa na shirika la habari la Saudi Arabia imekariri Wizara ya Hajj na Umrah kutoa tangazo hilo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters taarifa imesema Ibada ya Hijja mwaka huu itaanza katikati ya mwezi Julai na itakuwa kwa watu wenye umri wa miaka 18 mpaka 65. Wale watakaoshiriki ibadah hii lazima wapatiwe chanjo, wizara imesema.
Chanzo cha Habari : Reuters