Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 21:01

Saudi Arabia yaondoa vikwazo dhidi ya Qatar


Waziri wa mambo ya nje wa Kuwait Ahmad Nasser al-Sabah akizungumza na waandishi wa habari mjini Amaan Jordan Oct.19, 2020 .
Waziri wa mambo ya nje wa Kuwait Ahmad Nasser al-Sabah akizungumza na waandishi wa habari mjini Amaan Jordan Oct.19, 2020 .

Saudi Arabia itaondoa zuio la muda mrefu kwa Qatar, kulingana na Wizara ya Mambo ya nje ya Kuwait.

Waziri wa Mambo ya nje wa Kuwait Ahmad Nasser al-Sabah alitangaza makubaliano hayo kwenye Televisheni ya Kuwait Jumatatu, akisema "Makubaliano yamefikiwa kufungua anga na mipaka ya ardhi na bahari kati ya Saudi Arabia na Qatar kuanzia jioni hii.

Alisema makubaliano hayo yatasainiwa katika mkutano wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba (GCC) huko Saudi Arabia Jumanne.
Mfalme wa Saudi Arabia Salman ndiye atakayeongoza mkutano huo na kiongozi wa Qatar sasa anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo kwa mara ya kwanza tangu mipaka ilipofungwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

Mzozo wa kidiplomasia ulianza mnamo mwaka 2017 wakati Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, Bahrain na Misri zilipokata uhusiano wa kidiplomasia, biashara na usafiri na Qatar.

Nchi hizo nne zilishutumu Qatar kwa kuunga mkono ugaidi, shutuma ambazo Doha imekanusha.

Imetayarishwa na Sunday Shomari, VOA,Washington DC

XS
SM
MD
LG