Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:24

NATO kujadili mkakati wake Brussels Jumatatu


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, katikati, na viongozi wengine saba wakiwa katika mkutano wa G7 huko Cornwall, Uingereza, Juni 12, 2021.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, katikati, na viongozi wengine saba wakiwa katika mkutano wa G7 huko Cornwall, Uingereza, Juni 12, 2021.

Muungano wa NATO umepanga kujadili dhana ya mkakati wake wakati viongozi wa muungano huo pamoja na Rais wa Marekani, Joe Biden watakapokutana Jumatatu mjini Brussels. 

NATO mara mwisho kuufanyia marekebisho waraka wake wa malengo ilikuwa mwaka 2010.

Vitisho vya usalama na changamoto inazoukabili muungano huo zimebadilika tangu wakati huo, kwa mujibu wa katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg.

Kwa mfano katika dhana ya mkakati wa sasa, China haijatajwa hata mara moja. Mabadiliko ya hali ya hewa hayatajwi kabisa, na kwa hakika uhusiano wetu na Russia ulikuwa katika sehemu tofauti ukilinganisha na hivi tulivyo leo, Stoltenberg amewaambia wanahabari.

Kwa upande wake utawala wa Rais wa Marekani ulisema Jumamosi utatangaza mkakati wa ufadhili wa miundombinu kwa nchi za kipato cha chini na cha kati.

Mkakati huo ambao umetengenezwa kushindana na ule wa hasimu wake China unaojulikana kama Belt and Road Initiative.

Juhudi hiyo itaitwa, “Build Back Better for the World,” umezinduliwa leo Jumamosi pamoja na washirika wa G7 katika mkutano unaofanyika Cornwall, Uingereza.

Chanzo cha Habari : VOA News

XS
SM
MD
LG