Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:58

London : Maandalizi ya ajenda ya mkutano wa G7 kukamilika leo


Mawaziri wa mataifa 7 tajiri duniani G7 wakiwa katika ukumbi wa mkutano kabla ya kuanza kakao cha mawaziri hao cha ana kwa ana London, Jumatano, Mei 5, 2021. (Ben Stansall/Pool Photo via AP)
Mawaziri wa mataifa 7 tajiri duniani G7 wakiwa katika ukumbi wa mkutano kabla ya kuanza kakao cha mawaziri hao cha ana kwa ana London, Jumatano, Mei 5, 2021. (Ben Stansall/Pool Photo via AP)

Mawaziri wa mataifa 7 tajiri duniani G7, wanamaliza mazungumzo yao ya siku mbili, mjini London, Jumatano, wakitayarisha ajenda ya mkutano wa viongozi wa mataifa hayo utakaofanyika mwezi Juni.

Mkutano huo wa kwanza wa ana kwa ana unazungumzia suala la chanjo leo baada ya kuzungumzia namna ya kukabiliana na kuongezeka kwa ushawishi wa China duniani na uchokozi wa Rashia pamoja na masuala ya migogoro katika baadhi ya nchi za afrika hasa Ethiopia na Somalia.

Mkutano huo pia ulikabiliwa na kitisho pale ujumbe wa India ulipotangaza kwamba wajumbe wake wawili wamepimwa na kupatikana na virusi vya corona.

Hofu ilizuka pale Waziri wa Mambo ya Nje wa India Subrahmanyam Jaishankar kutangaza kwamba hatohudhuria binafsi wala ujumbe wake kwenye vikao vya leo akichukua tahadhari baada ya wajumbe wake wawili kupimwa na kupatikana wameambukizwa na virusi vya Corona.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi 7 Tajiri duniani wakutana ana kwa ana London.
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi 7 Tajiri duniani wakutana ana kwa ana London.

India si mwanachama wa G7 lakini imealikwa na Korea kusini, Australia na Afrika Kusini kama wageni kuhudhuria vikao vya hii leo.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson aliyetarajiwa kukutana na Jaishankar leo akiulizwa ikiwa ilikuwa ni makosa kuitisha mkutano huo wa ana kwa ana wakati huu, amesema ni muhimu kujaribu kuanza kufanya kazi kama ilivyokua kawaida.

Waziri Mkuu wa Uingerezsa Boris Johnson, kulia, akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ofisini kwake 10 Downing Street, London, Mei 4, 2021.
Waziri Mkuu wa Uingerezsa Boris Johnson, kulia, akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ofisini kwake 10 Downing Street, London, Mei 4, 2021.

Johnson alisema :Tuna uhusiano muhimu sana na India na washirika wetu wa G7. Ninavyofahamu kilichotokea watu waliohusika wamejitenga kutoka wengine. Na hivyo mambo yamedhibitiwa. Mimi nitakutana na Waziri wa Mambo ya Nje kupitia mtandao wa Zoom."

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje walizungumzia janga linaloikumba India kwa wakati huu na jinsi mataifa hayo yataweza kuisaidia nchi hiyo kwa vifaa muhimu vinavyohitajika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Dominic Raab mwenyeji wa mkutano, anasema mawaziri walijadili pia juu ya namna ya kuimarisha mpango wa Shirika la Afya Duniani COVAX kuzipatia chanjo mataifa yanayoendelea.

Raab alieleza : "Ninadhani COVAX na uwezo wa kuigharimia, ili chanjo ziweze kupelekwa kwa nchi zilizo katika hali ya hatari, na nini la kufanya kuhusiana na chanjo ziada tulizonazo ni masuala muhimu. Na ni nafasi nzuri kwa G7 kuwepo pamoja hapa na washirika wetu kuzungumzia mambo haya yote na kuweza kupata majibu chanya."

Mawaziri hao wa mataifa Tajiri duniani wanatayarisha ajenda ya mazungumzo ya viongozi wa G7 mwezi ujao huko Cornwall Uingereza ambao pia watakutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza na kuzungumzia changa moto mbalimbali zinazokabili dunia kwa wakati huu.

Waziri Raaba amesema kwamba mikutano hii inaonyesha kwamba diplomasia imerudi tena kufanya kazi.

Raab ameongeza : "Na ninadhani hali hii inaonyesha jinsi ilivyo muhimu sisi kukutana na kukabiliana na changamoto zilizoko kote duniani kwa wakati huu, changamoto zote za kimataifa zinazotukabili ili kuwezesha mataifa kukutana tena na kufanya kazi pamoja."

Kando ya mkutano mkuu mawaziri wamekuwa wakikutana kwa mazungumzo juu ya ushirikiano wa nchi na nchi, na mwenyeji wa mazungumzo Uingereza ambayo ni mwenyekiti wa G7 kwa mwaka 2020, inasema hii ni nafasi ya kuonyesha umoja unaohitajika sana wakati huu wa kukabiliana na changamoto na vitisho vinavyojitokeza duniani.

XS
SM
MD
LG