Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:53

Uingereza yatangaza mapendekezo yake katika mazungumzo watakayofanya na EU


Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel, kushoto, akizungumza na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kulia, na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel, wapili kulia, wakati wa mkutano wa pembeni wa Umoja wa Ulaya, EU, huko Brussels, Belgium, Feb. 20, 2020.
Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel, kushoto, akizungumza na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kulia, na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel, wapili kulia, wakati wa mkutano wa pembeni wa Umoja wa Ulaya, EU, huko Brussels, Belgium, Feb. 20, 2020.

Serikali ya Uingereza imetangaza mapendekezo yake kwa ajili ya mazungumzo ya biashara na Umoja wa Ulaya (EU).

Wakati huo huo serikali hiyo imetishia itaondoka kwenye meza ya mazungumzo ikiwa hakuna maendeleo yatapatikana katika muda wa miezi minne.

Hofu ya kuwepo mvutano

Wachambuzi wanasema pande hizo mbili zinaonekana zitakuwa na mvutano mkubwa kaika duru hiyo ya kwanza ya mazungumzo baada ya Uingereza kujiondoa kutoka EU mwezi uliyopita.

Maafisa wa Uingereza na Umoja wa Ulaya wanasema wanataka kufikia makubaliano ya biashara huru kwa maelewano, lakini tayari kuna maoni yanayotofautiana sana yanayojitokeza juu ya ushindani wa haki utachukuliwa vipi kati ya pande hizo mbili.

Masharti ya EU

EU inaitaka Uingereza kukubali kufuata kanuni zilizopo katika Nyanja kuanzia msaada wa taifa hadi ulinzi wa mazingira pamoja na kuruhusu boti za uvuvi za nchi za ulaya kuingia katika bahari yake ikiwa makubaliano ya haki yatafikiwa.

Mvutano halisi unatokana na matakwa ya Uingereza kufikiwa mkataba wa biashara uliyo karibu sawa na ule kati ya EU na Canada.

EU imeshapinga pendekezo hilo ikieleza kwamba kwa vile Uingereza ni jirani wake itakuwa tishio kubwa kwa soko la Ulaya kwa vile itafanya biashara nyingi zaidi kuliko Canada.

EU inahofia Uingereza huenda ikapunguza bei za bidhaa zake kwa kupunguza viwango vyake, jambo ambalo Waziri Mkuu Boris Johnson anakanusha.

Johnson aeleza msimamo wake

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson : "Tutaendelea kushikilia viwango vya juu kabisa, kile tunachokitaka ni kutaambua na kuheshimu viwango vya juu vya kila kitu na kuweza kuingia katika masoko ya kila mmoja wetu."

Anaongeza : "Ninacho maanisha ni kwamba hatutoitaka Umoja wa Ulaya, EU, kufuata kila kitu, kila mabadiliko ya sheria za Uingereza, na hivyo hivyo Uingereza haitaki shinikizo lolote kutoka kwao.

Akizungumza na waandishi habari mjini Brussels baada ya kuchapishwa mapendekezo hayo msemaji wa kamisheni ya EU Dana Spinant anasema hataweza kutoa maoni yeyote hivi sasa hadi mazungumzo yataanza Jumatatu.

Kamisheni ya Ulaya yatoa ufafanuzi

Naye Dana Spinant, Msemaji wa Kamisheni ya Ulaya anaeleza : "Tutatafakari juu ya hati iliyochapishwa, lakini kwa hivi sasa hatuna maoni yoyote juu ya mapendekezo hayo. Hata kama hakuna maendeleo yanayopatikana tumejitayarisha. Lakini ni mapema mno kuzungumzia matokeo hata kabla ya kuanza majadiliano."

Uingereza ilijiondoa rasmi kutoka EU januari 31 lakini inalazimika kubaki kufuata kanuni za umoja huo hadi baada ya kipindi cha mpito kumalizika Disemba 31.

Kipindi hicho kinaweza kuongezwa kwa mwaka mmoja zaidi lakini Waziri Mkuu Johnson anasema nchi yake itajiondoa kabisa kutoka mfumo wa soko la EU hapo Januari mosi 2021. Hata hivyo inamatumaini ya kufikia makubaliano ya biashara kabla ya muda huo kumalizika.

XS
SM
MD
LG