Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 20:43

Kenya yaweka masharti kwa abiria wanaotoka au kupitia Uingereza


Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta

Mzozo kati ya Kenya na Uingereza umeendelea kutokota baada ya serikali ya taifa hilo la Afrika Mashariki kutangaza masharti mapya kwa abiria wanaotoka au kupitia Uingereza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara Mambo ya Nje ya Kenya, masharti hayo yataanza kutekelezwa kuanzia Aprili 9, 2021, ambayo ni siku ya Ijumaa.

Uamuzi huu unaonekana kama ulipizaji kisasi, kufuatia hatua ya Uingereza kupiga marufuku abiria wote wa ndege waliopitia au kutoka nchini Kenya.

Waziri Mkuu Boris Johnson
Waziri Mkuu Boris Johnson

Aidha taarifa hiyo inaeleza kwamba abiria kutoka Uingereza ni sharti wawe na vyeti vya kuonyesha kuwa hawana virusi vya Corona, na kwamba wamepata chanjo ya Covid-19, kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation.

Abiria hao pia wameagizwa kujitenga na watu wengine kwa siku saba baada ya kuwasili nchini.
Ndege za mizigo hata hivyo, hazijaorodheshwa kwenye marufuku hiyo, ila marubani na wafanyakazi wake wengine, ni sharti wawe na vyeti vinavyohitajika, vya kuonyesha hawana virusi, na kwamba wamepokea chanjo ya Covid-19.
Siku ya Alhamisi, Uingereza iliiongeza Kenya, Ufilipino na Bangladesh, kwenye orodha ya nchi ambazo, abiria wake hawataruhusiwa kuingia nchini.

XS
SM
MD
LG