Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 11:02

Wabunge Uganda wataka hatua zichukuliwe dhidi ya Kenya


FILE - Wabunge wa Uganda wakiwa katika kikao Kampala, Uganda, Sept. 21, 2017.
FILE - Wabunge wa Uganda wakiwa katika kikao Kampala, Uganda, Sept. 21, 2017.

Mzozo wa kibiashara kati ya Kenya na Uganda, umechukua mwelekeo mpya, wakati bunge likikutana kujadili marufuku iliyotangazwa na Kenya, ya uagizaji wa mahindi kutoka nchi jirani, ikiwemo Uganda.

Wabunge hao waliishutumu Kenya kwa kile walichokiita “hulka ya unyanyasaji katika ukanda wa Afrika Mashariki,” na kutaka hatua za kulipiza kisasi zichukuliwe, kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor.

Wabunge pia waliitaka serikali kueleza ni kwa nini Uganda inapaswa kuendelea na juhudi za kuimarisha ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki “wakati majirani zake, wanadumaza itifaki ya Soko la Pamoja,”ambayo, imetiwa saini na nchi wanachama.

Mwishoni mwa wiki, serikali ya Kenya kupitia Mamlaka ya Kilimo na Chakula ilitangaza kupiga marufuku mahindi ya Uganda na Tanzania kwa kile ilichosema ni sababu zinazohusiana na afya. Ilisema kwamba uchunguzi ulidhihirisha kuwepo kwa kiwango cha juu cha kemikali ya mycotoxins, ambacho si salama kwa afya ya binadamu.

Mbunge wa Manispaa ya Busia Geofrey Macho alisema angalau watu zaidi ya 5,000,000, wakiwemo wakulima na wafanyabiashara, watapata hasara kutokana na marufuku hiyo, na kuitaka Uganda kupiga marufuku bidhaa hizo kutoka Kenya, akidai kwamba zinatumia kemikali nyingi kuliko Uganda.

XS
SM
MD
LG