Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:09

Kenyatta; Mazingira yanaweza kutoa suluhisho kwa changamoto za kibinadamu


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akifunga mkutano wa mazingira amesisitiza shida nyingi za mazingira zinazoikabili Dunia zinaweza kutoa suluhisho kwa changamoto nyingi tunazokabiliana nazo kama binadamu

Mawaziri wa mazingira na viongozi wengine kutoka zaidi ya mataifa 150 wamemaliza kikao cha siku mbili kwa njia ya video katika mkutano wa tano wa mazingira wa Umoja wa Mataifa-UNEA-5 ambapo bunge lilionya kuwa ulimwengu upo hatarini kwa majanga mapya kama hatutabadilisha namna tunavyotunza mazingira ya asili.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amefunga mkutano huo kwa matamshi yanayosisitiza shida nyingi za mazingira zinazoikabili Dunia lakini ameongeza kuwa mazingira yanaweza kutoa suluhisho kwa changamoto nyingi tunazokabiliana nazo kama binadamu.

Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya
Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya

Mkutano huo ulihudhuriwa na maelfu ya washiriki wa mtandao, wakiwemo zaidi ya wajumbe 1,500 kutoka mataifa 153 wanachama wa Umoja wa Mataifa na mawaziri zaidi ya 60 wa mazingira.

Bunge ambalo lilionekana moja kwa moja pia lilikubaliana juu ya mambo muhimu ya kazi za UNEP kuanzia sherehe za miaka 50 ya maadhimisho ya UNEP mwaka 2022 na kufanya mazungumzo na uongozi mahala ambapo nchi wanachama walielezea namna ya kujenga ulimwengu wenye nguvu na unaojumuisha hali ya baadae ya janga hili.

XS
SM
MD
LG