Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 01:00

Kenyatta ndiye mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Jumamosi Februari 27, 2021
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Jumamosi Februari 27, 2021

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Jumamosi alikabidhiwa uenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika Mashariki (EAC) na mwenyekiti anayeondoka, Rais wa Rwanda, Paul Kagame.

Hii ni kufuatia mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao uliohudhuriwa na viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Dkt Peter Mathuki, raia wa Kenya, sasa ndiye katibu mkuu mpya wa Jumuiya hiyo, akichukua nafasi ya Balozi Liberate Mfumukeko, raia wa Burundi, ambaye amekamilisha muhula wake.

Kabla ya uteuzi huo, Mathuki alikuwa mkurugenzi mtendaji wa baraza la Biashara la nchi za Afrika mashariki.

Kwenye mkutano huo, ambao pia ulihudhuriwa na rais Paul Kagame wa Rwanda na makamu rais wa Tanzania tanzania Samia Suluhu Hassan, viongozi wa nchi wanachama walisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiano.

Aidha, mmoja wa majaji wapya wa mahakama ya haki ya Afrika Mashariki, Kathurima M’Inoti aliapishwa.

-Imetayarishwa na Asiraji Mvungi, Arusha, Tanzania

XS
SM
MD
LG