Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 01:24

Kenya yaipa UNHCR siku 14 kufunga kambi ya Daadab na Kakuma


Wakimbizi wakipokea msaada katika kambi ya Kakuma wakati huu wa janga la coronaKenya, Aprili 2020 (Photo: Samuel Otieno/Twitter @UNOCHA)
Wakimbizi wakipokea msaada katika kambi ya Kakuma wakati huu wa janga la coronaKenya, Aprili 2020 (Photo: Samuel Otieno/Twitter @UNOCHA)

Kenya imeamuru kambi mbili kubwa zaidi za wakimbizi nchini humo zifungwe ndani ya kipindi cha wiki mbili.

Serikali ya nchi hiyo imelipatia shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi, UNHCR, siku kumi na nne kufunga kambi za Dadaab na Kakuma, zinazowahifadhi wakimbizi wapatao laki tano.

Imesema kinyume cha hivyo, wakimbizi hao watasafirishwa hadi kwenye mpaka wake na Somalia.

Ujumbe huo uliwasilishwa Jumanne na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Fred Matiang'i alipokutana na maafisa wa shirika hilo la wakimbizi kwenye afisi yake mjini Nairobi.

Fred Matiang’i
Fred Matiang’i


"Hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu za usalama wa kitaifa," alisema Matiang'i.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, Matiang’i alimwambia mwakilishi wa UNHCR nchini Kenya, Fathiaa Abdala, kwamba hakutakuwa na mjadala wowote kuhusu suala hilo.

Mnamo mwaka wa 2013, serikali ya Kenya ilikuwa imekubali kuwahamisha wakimbizi hao kwa awamu tatu, lakini kufikia sasa, ni wakimbizi 14,000 pekee, ambao wamehamishwa.

Kati ya masuala mengine, serikali imekuwa ikilalamika kwamba, licha ya ahadi za mara kwa mara, za misaada kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, kwa kiasi kikubwa imeendela kuubeba mzigo wa kuwahifadhi wakimbizi hao peke yake.

Kenya ilitaka kuzifunga kambi hizo mwaka wa 2016 kufuatia mashambulizi ya liyoaminika kutekelezwa na wanamgambo wa asili ya Somalia.

Kambi hizo zimekuwepo tangu maika ya tisini wakati ambapo vita vya wenyewe kwa wenyewe vilianza nchini Somalia, na ambavyo vinaendelea hadi sasa. Wengi wa wakimbizi hao ni raia wa Somalia.

XS
SM
MD
LG