Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 03:11

Uingereza yaeleza nia yake ya kufungua fursa za uhamiaji kwa Afrika


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amewambia viongozi wa nchi za Afrika, Uingereza itakuwa mkarimu zaidi kwa wahamaiji kutoka bara lao baada ya Brexit, wakati akifungua mkutano wenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya nchi yake na Afrika.

Boris ameahidi kwamba mfumo wa uhamiaji wa nchi yake utabadilishwa na kuruhusu watu wenye ujuzi wa teknolojia na wale wanaotaka kusoma katika vyuo vikuu watakaribishwa.

Kiongozi huyo aliahidi pia kukomesha kabisa uwekezaji kutoka serikali ya Uingereza katika uchimbaji makaa au mitambo ya umeme inayotumia makaa katika nchi za nje, akiongeza London itazingatia katika kuunga mkono miradi ya nishati mbadala.

Viongozi kutokia mataifa 21 ya Afrika wanahudhuria mkutano huo ambao unatarajiwa kutoa tangazo muhimu la kuimarisha biashara na mikataba ya biashara yenye thamani ya mabilioni ya dola.

Miongoni mwa viongozi wanaohudhuria kikao cha leo mjini London ni Rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Muhamad Buhari wa Nigeria na Nana Akufo Addo wa Ghana.

Serikali ya Uingereza imesema kwamba baada ya kikao hicho, inatarajia kuwepo mikataba yenye thamani ya dola bilioni 6.5 kati yake na mataifa ya Afrika.

XS
SM
MD
LG