Gazeti la Sunday Nation la Kenya limeripoti, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters kikosi hicho maalumu ni kwa ajili ya kusaidia eneo hilo katika kukabiliana na ugaidi.
Katika barua yake kwa Bunge la Marekani ambayo gazeti hilo limeiona, Rais Biden amesema kwamba ameidhinisha upelekaji wa kikosi cha operesheni maalum huko Kenya, ambacho kilitarajiwa kushirikiana na jeshi la Kenya katika kupambana na al-Shabaab.
Idadi ya wanajeshi wanaokwenda huko haijatajwa. Upelekaji wa wanajeshi unatarajiwa kuboresha usalama kwa Kenya, ambayo katika miaka ya karibuni imekumbwa na mashambulizi kadhaa kutoka kwa Al shabaab.
Kundi hilo lenye makao yake nchini Somalia linajulikana kuwa lina wanaowaonea huruma nchini Kenya.
Vyanzo vya Habari : Sunday Nation, Reuters