Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:11

Shambulizi la kujitoa muhanga Somalia laua gavana na wengine wanne


Ramani ya Somalia na Puntland
Ramani ya Somalia na Puntland

Mlipuko wa bomu la kujitoa muhanga katika eneo la kati la Somalia limeua watu watano akiwemo gavana wa mkoa huo Jumapili, maafisa wameiambia Sauti ya Amerika (VOA).

Gavana huyo wa uongozi wa Puntland mkoa wa Mudug Ahmed Muse Nur, kaka yake na walinzi wake wawili waliuawa baada ya mtu aliyejitoa muhanga akiendesha gari aina ya Toyota Noah kuigonga gari yao katika mji wa Galkayo, kilomita 600 kaskazini ya Mogadishu.

Raia aliyekuwa pembeni ya barabara pia aliuawa. Mtu aliyejitoa muhanga alipoteza maisha, maafisa wamesema. Watu wengine 4 walijeruhiwa akiwemo dereva wa gavana.

Meya Sahid Mohamud Ali ameiambia VOA kuwa gavana huyo alikufa papo hapo pamoja na walinzi wake na kaka yake.

“Gari iliogonga gari ya gavana ilikuwa imejaa vilipuzi kwa ajili ya kujitoa muhanga,” Ali amesema.

Nur alikuwa ameteuliwa katika nafasi ya ugavana Mei, 2019. Siku za nyuma aliwahi kutumikia wadhifa wa naibu gavana na alikuwa akijulikana kwa uzoefu wake wa siasa za eneo.

Kikundi cha al-Shabaab kimedai kuhusika na mlipuko huo.

Nur ni gavana wa pili kutoka utawala wa Puntland kuuawa katika shambulizi la bomu la kujitoa muhanga katika kipindi cha miezi miwili. Mnamo Machi 29, gavana wa mkoa wa Nugal Abdisalam Hassan Hersi aliuawa kutokana na majeraha yaliyotokana na shambulizi la bomu la kujitoa muhanga katika mji wa Garowe.

XS
SM
MD
LG