Kituo hicho kinachotumiwa na vikosi vya Marekani vinavyo pambana na ugaidi vilivyoko nchini Kenya kabla ya kuingia alfajiri Jumapili.
Wingu kubwa la moshi mweusi liliweza kuonekana likipanda angani kutoka katika uwanja wa ndege wa Manda Bay katika pwani ya mji wa Lamu, katika mpaka wa Kenya na Somalia.
Kwa mujibu wa jeshi hilo, shambulizi hilo pia liliharibu ndege kadhaa za Marekani na magari kabla ya kulidhibiti. Ilikuwa ni shambulizi la kwanza lililohusishwa na kikundi cha al-Qaida dhidi ya vikosi vya Marekani katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Msemaji wa jeshi la Kenya amesema katika tamko lake kuwa washambuliaji watano waliuawa.
Kikosi cha Jeshi la Marekani Afrika (AFRICOM) kimethibitisha baadhi ya moshi huo inawezekana ulitokana na uharibifu wa vifaa katika kituo hicho.
Al-Shabaab imesema katika tamko lake kwamba ilikuwa inashikilia sehemu ya kituo hicho cha kijeshi, na ilikuwa imesababisha vifo katika shambulizi hilo.