Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:22

Wasomali wamuomba Biden kubadili uamuzi wa Trump kuondoa majeshi


Rais Donald Trump (kulia) na Rais mteule Joe Biden.
Rais Donald Trump (kulia) na Rais mteule Joe Biden.

Uamuzi wa Rais Donald Trump kuwaondoa wanajeshi wa Marekani nchini Somalia katika siku za mwisho za urais wake, umechochea malalamiko kutoka kwa baadhi ya Wasomali, ambao wamemuomba rais ajaye Joe Biden kubadili uamuzi huo.

"Uamuzi wa Marekani kuondoa wanajeshi wake nchini Somalia katika kipindi hiki muhimu cha mafanikio katika mapamano dhidi ya al-Shabaab na mtandao wao wa kigaidi ulimwenguni ni jambo la kusikitisha sana,” Seneta Ayub Ismail Yusuf ameliambia shirika la habari la Reuters katika taarifa, akilitaja al-Qaeda likihusishwa na uasi wa al-Shabaab.

FILE - Wapiganaji wa al-Shabab wakiwa nje ya mji wa Mogadishu, Somalia, Machi 5, 2012.
FILE - Wapiganaji wa al-Shabab wakiwa nje ya mji wa Mogadishu, Somalia, Machi 5, 2012.

"Wanajeshi wa Marekani wamekuwa na mchango mkubwa na mafanikio mazuri katika mafunzo na operesheni kwa wanajeshi wa Somalia,” amesema Yusuf, mjumbe katika kamati ya mambo ya nje kwenye baraza la senate la Somalia.

Serikali ya Somalia haikuweza kupatikana haraka kutoa maoni yake mapema Jumamosi kuhusu uamuzi wa Ijumaa wa kuondoa takriban wanajeshi wote 700 wa Marekani ifikapo Januari 15.

Serikali tete ya Somalia inayotambuliwa kimataifa inatarajiwa kuitisha uchaguzi wa bunge mwezi huu na uchaguzi wa kitaifa mapema mwezi Februari, ambapo kikosi cha ulinzi wa amani cha Umoja wa Afrika chenye wanajeshi takriban 17,000 kitakuwepo kushuhudia zoezi hilo.

Wanajeshi wa Marekani wamekuwepo nchini Somalia, kwa kiasi kikubwa kuwaunga mkono kikosi maalum cha Somalia kinachojulikana kama Danab katika operesheni zake dhidi ya al-Shabaab, ambayo mashambulizi yake katika mataifa ya Kenya na Uganda yamesababisha vifo vya mamia ya raia, wakiwemo Wamarekani.

Wanajeshi wa Marekani wa kikosi cha kwanza wakiwa nchini Somalia
Wanajeshi wa Marekani wa kikosi cha kwanza wakiwa nchini Somalia

Kuyasaidia Majeshi ya Somalia

Danab inafanya jitihada kubwa kwasababy majeshi ya kawaida mara nyingi yanakuwa na mafunzo duni na vifaa vichache, mara kwa mara yakiondoa kwenye vituo vyao au wanajikuta katika mapambano ya madaraka kati ya serikali za kitaifa na kieneo.

Kama kujiondoa huko kutakuwa kwa kudumu, “itakuwa na athari kubwa kwa juhudi za kukabiliana na ugaidi,” amesema kanali Ahmed Abdullahi Sheikh, ambaye alihudumu kwa miaka mitatu mpaka mwaka 2019 kama kamanda wa Danab.

Alipigana sambamba na majeshi ya Marekani, amesema, na wakati wa uongozi wake wamarekani wawili na zaidi ya wanajeshi 100 wa kikosi chake walikura. Wote majeshi ya Marekani na Somalia yamepinga kuondolewa kwa wanajeshi hao, amesema.

Program ya Marekani ya kupanua Danab na kufikia wanajeshi 3,000 ilitakiwa kuendelea mpaka mwaka 2027, Sheikh amesema, lakini hali ya siku za usoni haiko wazi.

Mashambulizi ya anga huenda yakaendelea kutoka kwenye kambi za kijeshi nchini Kenya na Djibouti, ambazo pia zitatoa fursa ya operesheni za kuvuka mpaka. Kundi la kutetea haki, Amnesty International anasema mashambulizi ya anga yameua takriban raia 16 katika muda wa miaka mitatu iliyopita.

Kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani kunakuja katika wakati ambako hali si shwari katika eneo hilo. Ethiopia, ambayo ni mchangiaji mkubwa wa wanajeshi katika jeshi la ulinzi wa amani na ina maelfu zaidi ya wanajeshi wake nchini Somalia, imegubikwa na mzozo wa ndani ambao ulizuka mapema mwezi Novemba. Imechukua silaha za mamia ya walinzi wake wa amani.

Somalia imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 1991, lakini kuingia kwa jeshi la ulinzi wa amani mwaka 2008 kumesaidia kuimarisha muundo wa serikali ambao uliruhusu mageuzi ya pole pole ya kijeshi, kama vile mfumo wa alama vidole ili kuwalipa wanajeshi na kuunda kwa kikosi cha Danab.

Lakini matatizo mengi na jeshi la Somalia bado yapo, ikiwemo rushwa na uingiliaji kati wa kisiasa. Pengine kuondoka kwa wanajeshi hao kutailazimisha Somalia kukabiliana nao, amesema Sheikh, au pengine itaifanya hali kuwa mbaya zaidi.

XS
SM
MD
LG