Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:37

Mashirika ya kimataifa yasisitiza usalama wa raia Somalia


Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za kibinadamu yamewasihi wanajeshi wa Ethiopia kuzingatia zaidi usalama wa raia katika eneo la Tigray wakati muda uliotangazwa na waziri mkuu Abiy Ahmed wa saa 72 kwa vikosi vya Tigray kujisalimisha, unakaribia kumalizika.

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, alitoa muda wa saa 72 kwa vikozi vya usalama vya Tigray kujisalimisha, la sivyo wakabiliwe na mashambulizi makali kutoka kwa wanajeshi wa serikali.

Tangazo hilo la jumapili, limeongeza mgogoro katika vita hivyo vya wiki nzima ambavyo vimesababisha vifo vya mamia ya watu.

Taarifa ya shirika la Amnesty international imesema kwamba inakumbusha kila pande husika katika mgogoro huo kuwa mashambulizi dhidi ya raia na mali zao hayakubaliki chini ya sheria ya kimataifa kuhusu haki za binadamu.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kwamba hatua hiyo ni uhalifu wa kivita.

Taarifa ya umoja wa mataifa

Umoja wa mataifa umesema Jumatatu kwamba zaidi ya watu 30,000 wamekimbia Ethiopia na kuingia Sudan kutokana na vita hivyo.

Umoja wa mataifa unataka raia kupewa ulinzi, ukiongezea kwamba kuna haja ya pande husika katika vita hivyo kuhakikisha kwamba raia wanaruhusiwa kutoka sehemu moja hadi nyingine ikiwemo kuvuka mpaka kwa njia salama wanapokimbia mapigano hayo.

Mawasiliano ya simu na huduma ya internet vimekatwa katika eneo la Tigray na kufanya vigumu kwa waandishi wa habari kujua idadi kamili ya watu ambao wamekufa kutokana na vita hivyo.

Eneo la Tigray, lililo kaskazini mwa Ethiopia, lina majimbo tisa.

Hali ya wasiwasi imekuwa ikiongezeka katika eneo hilo tangu Septemba 9 wakati viongozi wa Tigray walipopuuza amri ya waziri mkuu Abiy Ahmed ya kutoandaa uchaguzi wakati huu wa janga la virusi vya Corona.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG