Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:10

Ethiopia yaahirisha uchaguzi katika majimbo mawili

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed. REUTERS/Tiksa Negeri/File Photo
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed. REUTERS/Tiksa Negeri/File Photo

Tume ya uchaguzi ya Ethiopia imeahirisha kufanyika uchaguzi hadi mwezi wa Septemba katika majimbo mawili ya Somali na Harari.

Upigaji kura uliyotarajiwa kufanyika katika muda wa siku 10 zijazo hautafanyika pia katika jimbo la Tigray ambako kuna mzozo unaoendelea kwa wakati huu.

Mwanamke akisubiri katika mstari kupata msaada wa chakula, katika shule ya msingi ya Tsehaye, ambacho kimefanywa ni kituo cha muda cha watu waliolazimika kukimbia maeneo yao kutokana na vita, katika mji wa Shire, Mkoa wa Tigray, Ethiopia, Machi 15, 2021.

Maafisa wa uchaguzi wanasema kasoro za upigaji kura na matatizo ya kuchapisha vyeti vya kura yamesababisha kucheleweshwa kufanyika uchaguzi huo.

Shirika la habari la Uingereza, Reuters limemnukuu mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Birtukan Mideksa akisema kwamba katika baadhi ya wilaya uchaguzi utafanyika mnamo duru ya pili hapo Septemba 6.

Hakuna tarehe iliyotajwa kwa ajili ya uchaguzi wa Tigray. Uchaguzi mkuu ulipangwa kufanyika mwezi Agosti mwaka 2020, lakini uliahirishwa kutokana na janga la virusi vya corona.

Chanzo cha Habari : Reuters

XS
SM
MD
LG