Hayo amesyasema Jumatatu wakati akihutubia wanahabari na kuongeza kuwa takriban watu milioni tano kutoka eneo hilo wanahitaji misaada ya dharura na hasa chakula.
Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Novemba mwaka uliyopita alituma vikosi vya serikali kuu kwenye eneo hilo akidai kuwa wapiganaji kutoka chama cha Tigray People's Liberation, TPLF walikuwa wameshambulia kambi za jeshi.
Kiongozi huyo ambaye pia aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel alitangaza ushindi baadaye mwezi huo baada ya wanajeshi wake kuchukua udhibiti wa mji mkuu wa Tigray, Mekele.
Hata hivyo mapigano yanaendelea miezi 6 baadaye huku kukiwa na madai ya mauwaji pamoja na ubakaji kutoka kwa viosi vya serikali pamoja na vile kutoka nchi jirani ya Eritrea.