Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:33

Blinken:Serikali ya Marekani ina wasi wasi kuhusu mzozo unaoendelea huko Ethiopia


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken

Watu wa Tigray wanaendelea kuathiriwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, manyanyaso, ukatili na misaada ya haraka ya kibinadamu imezuiliwa kufika huko na majeshi ya Ethipia na Tigray

Waziri wa mambo ya nje, Antony Blinken alisema serikali ya Marekani ina wasi wasi mkubwa kuhusu kuendelea kwa mzozo katika mkoa wa Tigray nchini Ethiopia pamoja na vitisho vingine kwa utaifa, umoja wa kitaifa na uadilifu wa Ethiopia.

Watu wa Tigray wanaendelea kuathiriwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, manyanyaso, ukatili na misaada ya haraka ya kibinadamu imezuiliwa kufika huko na majeshi ya Ethipia na Tigray pamoja na makundi mengine yenye silaha, taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema.

Licha ya kujihusisha kidiplomasia pande zinazohusika na mzozo huko Tigray hazijachukua hatua zinazohitajika kumaliza chuki au kutafuta suluhisho la amani kwa mzozo huo wa kisiasa. Waziri Blinken alisema Marekani inalaani vikali sana mauaji, kuondolewa kwa nguvu, manyanyaso ya kingono na manyanyaso mengine. Tumesikitishwa sana na uharibifu wa mali za raia ikiwemo vyanzo vya maji, hospitali na vifaa vya afya huko Tigray.

XS
SM
MD
LG