Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 05:45

Putin adai uhusiano kati ya Russia na Marekani uko chini mno


Rais Joe Biden (kushoto) na Rais Vladimir Putin
Rais Joe Biden (kushoto) na Rais Vladimir Putin

Rais wa Russia Vladimir Putin amesema katika mahojiano na NBC News kabla ya mkutano wake na Rais wa Marekani, Joe Biden wiki ijayo kuwa uhusiano wa Marekani na Russia uko katika kiwango cha chini mno hivi sasa.

Putin na Biden watakutana Geneva Jumatano. White House imesema Biden atazungumzia suala la mashambulizi ya kimtandao kutoka Russia, uchokozi wa Moscow dhidi ya Ukraine, na kuwafunga wapinzani na masuala mengine ambayo yametia dosari uhusiano wao.

Tuna uhusiano wa pamoja na huo umeshuka sana katika miaka ya karibuni, Putin amesema, kwa mujibu wa matamshi yaliyotafsiriwa na NBC katika mahojiano ambayo yalirushwa jana Ijumaa.

Putin amempongeza rais wa zamani Donald Trump kama mtu ambaye si wa kawaida, mwenye ujuzi na kusema Biden ni mwanasiasa wa siku nyingi ambaye ni tofauti kabisa na Trump.

Chanzo cha Habari : Reuters

XS
SM
MD
LG