Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:01

Rais Biden afanya ziara Ulaya


Rais wa Marekani Joe Biden akiandamana na mke wake Jill Biden muda mfupi baada ya kuwasili Uingereza
Rais wa Marekani Joe Biden akiandamana na mke wake Jill Biden muda mfupi baada ya kuwasili Uingereza

Rais wa Marekani Joe Biden Jumatano amefanya ziara yake ya kwanza barani Ulaya tangu kuchukua madaraka ambapo anatarajiwa kufanya mazungumzo ya ngazi ya juu na viongozi kadhaa wa mataifa ya magharibi, kabla ya kufanya kikao wiki ijayo na rais wa Russia Vladimir Putin mjini Geneva Uswizi.

Mara baada ya kutua Biden alihutubia vikosi vya marekani huko RFA Mildenhall Uingereza, na kuwaeleza kuwa “Tunawashukuru sana na kujivunia uwepo wenu.” Aliongeza kusema kuwa ameweka dhahiri kwamba Marekani itajibu vilivyo iwapo serikali ya Russia itajihusisha kwenye masuala hatarishi.

Biden aliongeza kusema kuwa wakati wa ziara yake atahakikishia washirika wa Marekani kushusu nafasi ya taifa lake kwenye masuala ya ulimwengu. Wakati akipanda ndege yake rasmi ya Airforce 1 hapa Marekani, Biden alisema kuwa lengo la ziara yake ni kuimarisha uhusiano na washirika wake huku pia akidhihirishia China na Russia kwamba uhusiano wa Marekani na Ulaya ni dhabiti.

Biden alisema kuwa atatangaza kuhusu mbinu mpya ya kutoa chanjo dhidi ya janga la corona kote ulimwenguni.

XS
SM
MD
LG