Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:33

Pakistan : Ajali ya basi yaua 23 na wengine 40 wajeruhiwa


Ajali ya basi katika jimbo la Balochistan, Pakistan, Ijumaa. (AP Photo/Younis Baloch)
Ajali ya basi katika jimbo la Balochistan, Pakistan, Ijumaa. (AP Photo/Younis Baloch)

Maafisa wa Pakistan wanasema watu 23 wamefariki na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa wakati basi lilipopinduka kusini magharibi mwa Pakistan na kuanguka kwenye bonde.

Ajali hiyo imetokea ijumaa hii katika wilaya ya Khuzdar kwenye jimbo la Balochistan.

Shirika la habari la Associated Press linaripoti kwamba abiria aliyeongea na shirika hilo amesema abiria walimtahadharisha dereva mara kadhaa kuendesha kwa uangalifu zaidi.

Abiria walikua mahujaji wakirudi huko Dadu katika jimbo la Sindh baada ya kutembelea kaburi la mtakatifu wa kisufi.

Basi lilikuwa limejaa, huku abiria wengine walikuwa wamepanda juu ya paa lake wakati lilipopinduka, amesema Bashir Ahmed, naibu kamishna katika wilaya ya Khuzdar.

Chanzo cha Habari : Associated Press

XS
SM
MD
LG