Pia rais ametoa wito kwa nchi za ulimwenguni kuchangia sehemu yao, kusaidia kumaliza janga hilo hatari, White House imesema.
Tangazo hilo la msaada wa chanjo, ambalo ndilo kubwa zaidi kuwahi kufanywa na nchi moja, linatolewa huku Biden akiwa kwenye ziara ya bara la Ulaya.
Rais wa Marekani anatarajiwa atakutana na viongozi wa nchi nyingine zenye nguvu zaidi duniani : Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Japan, katika mji wa Cornwall, nchhini Uingereza.
Ikulu ya Marekani imesema lengo la mchango huo, ni kuokoa maisha, na kutokomeza janga hilo, na kwamba itatoa mikakati ya hatua za ziada, katika siku zijazo.
Kampuni ya Marekani ya kutengeneza chanjo ya Pfizer, na ile ya Ujerumani ya BioNTech, zimethibitisha kwamba mwaka 2021, zitatoa dozi milioni 200, na zingine milioni 300, katika nusu ya kwanza ya mwaka 2022 ambazo Marekani itasambaza kwa nchi 92, zenye kipato cha chini, na pia kwa jumuiya ya Umoja wa Afrika.
Dozi ambazo zitatengenezwa na kampuni ya Pfizer, zitatolewa kwa bei nafuu.
Vyanzo : Mashirika mbalimbali ya habari