Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:58

Kibali maalum kutolewa kwa wasafiri wanaozuru nchi za EU


Bunge la Umoja wa Ulaya, Brussels
Bunge la Umoja wa Ulaya, Brussels

Wabunge wa Umoja wa Ulaya (EU) Jumatano wamepitisha kibali cha kusafiri kitakacho waruhusu wananchi wake kuingia katika mataifa ya Ulaya bila ya kuwekwa karantini.

Kibali hicho pia kitamuruhusu msafiri kuingia katika nchi hizo bila ya kufanyiwa vipimo zaidi vya virusi vya corona, na kufungua njia ya cheti hicho cha usafiri kutumika kabla kuanza kipindi cha majira ya joto, vyanzo vya habari mbalimbali vimeripoti.

Cheti hicho kilicho subiriwa kwa hamu kubwa kikiwa na lengo la kusaidia sekta ya usafiri ya Ulaya wakati wa kipindi muhimu cha utalii ili kuepusha mdororo mwingine ulio sababishwa na marufuku za Covid -19 katika sekta hiyo.

Mataifa ambayo hutembelewa sana kama vile Ugiriki yameongoza shauri la kuwepo cheti maalumu kitakacho tolewa katika karatasi na kieletroniki ili kianze kufanya kazi.

Vyanzo : Mashirika mbalimbali ya habari

XS
SM
MD
LG