Akizungumza na waandishi habari mjini Porto Ureno ambako viongozi wa EU wamekutana ana kwa ana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kupitia video siku ya Jumamosi, Michel amesema kwamba wamekubaliana kuanzisha tena mazungumzo ya biashara na kulinda uwekezaji pamoja na kuimarishia ushirikiano kati yao.
Makubaliano hayo yatawezesha kuanzishwa tena mazungumzo yaliyokwama tangu 2007 kuhusu mkataba wa biashara huru kati ya pande mbili uliyositishwa mwaka 2013.
Wakati huo huo Mkuu wa Kamisheni ya Ulaya Ursala von der Leyen amesema viongozi hao wa EU wamefikia pia makubaliano huko Porto juu ya mkataba na makampuni ya dawa ya BioNtech na Pfizer kutenegenza dozi bilioni 1 na milioni 800 za chanjo ya kupambana na virusi vya corona kwa ajili ya matumizi kwenye Jumuia yao kwa kipindi cha mwake 2021hadi 2023.
Aidha viongozi hao waliitaka pia Marekani kuondoa vizuizi vya kusafirisha nje chanjo kwa ajili ya COVID-19 kabla ya kuzungumzia suala la kuondolewa hati miliki za chanjo.
Marekani na Uingereza ni miongoni mwa nchi zisizoruhusu kusafiorishwa nje dawa za kupambana na COVID-19 zilizotengeneza nchini humo.