Mkutano huo ni ishara kwamba viongozi hao wanachukulia kitisho cha janga la COVID-19 kinapungua kutokana na kuharakishwa kwa mpango wa kuwachanja raia wao.
Mazungumzo yao yatazingatia zaidi athari za janga hilo katika fani za huduma za kijamii na ajira katika jumuia yao.
Viongozi wa EU watazungumzia pia pendekezo la Alhamisi lililotolewa na serikali ya Marekani kubadilishana habari za kiteknolojia kuhusu utengenezaji wa chanjo za COVID-19 ili kusaidia kukomesha kwa haraka janga hili.
Viongozi hao watakuwa pia na mazungumzo ambayo hayajawahi kufanyika kupitia mtandao wa video na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ambaye nchi yake inahitaji msaada mkubwa kukabiliana na maafa yanayotokea kutokana na kuongezeka kwa maabukizo.