Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza lengo jipya la chanjo ya kitaifa ya COVID-19 la asilimia 70 ya Wamarekani la kupokea chanjo moja ifikapo Julai 4 ikiashiria ni kitendo kipya cha kuirudisha nchi katika hali ya kawaida katika kuelekea maadhimisho ya kumbukumbu ya uhuru wa Marekani.
Hiyo inamaanisha kutoa karibu chanjo milioni 100 nyingine dozi za kwanza, wengine za pili katika siku 60 zijazo, rais alisema katika hotuba yake kutoka Ikulu Jumanne.
Karibu asilimia 40 ya watu wazima wa Marekani sasa wamepewa chanjo kamili dhidi ya COVID-19, kulingana na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa.
Maafisa wakuu wa utawala wanasema ikiwa asilimia 70 hadi 85 ya idadi ya watu wa Marekani watapewa chanjo, hiyo itasababisha kiwango cha chini cha maambukizi, na kuiweka nchi katika njia ya kurudi kwenye maisha ya kawaida.