Ripoti ya Wizara ya Kazi kuhusu ajira ambayo inatolewa Ijumaa itakuwa ya kwanza inayoonyesha mafanikio ya msaada wa afueni ya COVID-19 wa dola trillioni 1.9 uliyotolewa na utawala wa Rais Joe Biden, baada ya kuidhinishwa na bunge mwezi Machi.
Kulingana na utafiti wa wachumi wa shirika la habari la Reuters, ajira ziliongezeka kufikia 978,000 mwezi uliopita, baada ya kuongezeka hadi 916,000 mwezi Machi. Pamoja na hilo, watu millioni 7.5 bado hawana ajira ikilinganishwa na viwango vya mwezi Februari mwaka 2020.
Miezi 12 iliyopita, watu millioni 20.6 walipoteza ajira baada ya biashara nyingi kufungwa ili kupunguza maambukizi ya wimbi la kwanza la COVID-19.