Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:03

Biden aongeza uwezo wa Marekani kupokea wakimbizi


Familia za wakimbizi kutoka Mexico wakijisalimisha kwa walinzi wa mpakani wa Marekani.
Familia za wakimbizi kutoka Mexico wakijisalimisha kwa walinzi wa mpakani wa Marekani.

Rais wa Marekani Joe Biden, ambaye hapo awali aliamua kuacha idadi ya wakimbizi iliyowekwa na mtangulizi wake ambayo ilikuwa ni chini sana kihistoria ya kuruhusu wakimbizi wanaoingia kila mwaka, Jumatatu alitangaza kwamba anaongeza mara nne ya idadi hiyo mwaka huu.

“Ninarekebisha kiwango cha juu cha idadi ya kukubaliwa kwa wakimbizi kuingia ya kila mwaka ya Marekani hadi 62,500 kwa mwaka huu wa fedha," rais Biden alisema katika taarifa Jumatatu alasiri.

"Hii inafuta idadi ndogo ya kihistoria iliyowekwa na utawala uliopita ya wakimbizi 15,000, ambayo haikuonyesha maadili ya Marekani kama taifa linalopokea na kusaidia wakimbizi aliongeza Biden.

Biden aliendelea kusema kwamba kiwango cha idadi mpya ya udahili wa wakimbizi pia kitaimarisha juhudi ambazo tayari zinaendelea kupanua uwezo wa Marekani kupokea wakimbizi, ili waweze kufikia lengo la udahili wa wakimbizi 125,000 ambao anakusudia kuweka kwa mwaka ujao wa fedha.

Wiki mbili zilizopita, Ikulu ya Marekani ilitangaza kwamba kiwango cha mwaka huu wa fedha kitabaki wakimbizi 15,000, ambacho kiliwekwa na Rais wa zamani Donald Trump. Tangazo hilo lilikuja licha ya ahadi ya Biden kwamba baada ya kuapishwa kwake mwezi Januari atapanua mpango huo. Hatua hiyo ilisababisha kupingwa na wademokrat wenzake huko kwenye baraza la Congress, na pia watetezi wa wakimbizi.

XS
SM
MD
LG