Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 01:24

Marekani yakanusha madai ya Iran


Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price amesema akizungumza na waandishi wa habari. NICHOLAS KAMM / POOL / AFP
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price amesema akizungumza na waandishi wa habari. NICHOLAS KAMM / POOL / AFP

Marekani inakanusha ripoti kwenye televisheni ya serikali ya Irani kwamba Tehran imefikia makubaliano na Washington na Uingereza kuwaachilia huru wafungwa walio na uhusiano na Magharibi ili kupata mabilioni ya dola katika msaada mpya wa kiuchumi.

Ripoti kwamba mpango wa kubadilishana wafungwa umefikiwa sio kweli, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price alisema siku ya Jumapili. "Kama tulivyosema, kila wakati tunafuatilia kwa hali ya juu kesi za Wamarekani waliowekwa kizuizini au waliopotea nchini Iran. Hatutasimama hadi tuweze kuwaunganisha wote na familia zao."

Mkuu wa Utawala wa Ikulu ya Marekani Ron Klain pia alikanusha ripoti ya Irani katika kipindi cha "Face the Nation" cha CBS News, akisema, "Hakuna makubaliano yeyote ya kuwaachilia Wamarekani hawa wanne. Tunafanya bidii sana ilio waachiliwe huru”.

Televisheni ya serikali ya Irani ilinukuu chanzo cha habari kikisema,kuwa "Wamarekani walikubali kulipa dola bilioni 7 na kubadilishana Wairani wanne ambao walikuwa wakifanya kazi ili kuwaondolea vikwazo wapelelezi wanne wa Marekani ambao wametumikia sehemu ya vifungo vyao."

Iran inafahamika kuwashikilia Wamarekani wanne jela ikiwa ni pamoja na Baquer na Siamak Namazi, mwana mazingira Morad Tahbaz na mfanyabiashara Mmarekani mwenye asili ya Iran Emad Shargi.

XS
SM
MD
LG