Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 20:38

Bodi ya usimamizi yashikilia uamuzi wa kumzuia Trump kutumia Facebook


Trump bado kazuiwa kuweza kurudi Facebook lakini jopo linataka Facebook kuangalia upya adhabu hiyo.
Trump bado kazuiwa kuweza kurudi Facebook lakini jopo linataka Facebook kuangalia upya adhabu hiyo.

Bodi ya usimamizi ya Facebook siku ya Jumatano ilishikilia uamuzi wake wa kupiga marufuku Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kutuma maoni kwenye akaunti zake za Facebook na Instagram, hatua iliyowekwa baada ya kuchapisha maneno ya uchochezi wakati mamia ya wafuasi wake walipovamia bunge la Marekani mnamo Januari 6.

Jopo hilo la kujitegemea hata hivyo, liliacha wazi uwezekano kwamba Trump anaweza kurudi kwenye tovuti yao maarufu, akisema haikuwa sawa kwa Facebook kuweka adhabu isiyojulikana na isiyo na kipimo ya kusimamishwa kwa muda usiojulikana.

Jopo hilo la uangalizi liliwapa watendaji wa Facebook miezi sita kukagua tena "adhabu holela" iliyowekwa siku moja baada ya ghasia, wakati Trump alipowahimiza wafuasi wake kukabiliana na wabunge walipothibitisha ushindi wa uchaguzi wa Joe Biden.

Mapitio hayo yalisema watendaji wa Facebook wanapaswa kuamua juu ya adhabu nyingine inayoonyesha uzito wa ukiukaji na matarajio ya madhara ya baadaye.

Utawala wa Facebook ulijibu kwa kusema sasa utazingatia uamuzi wa bodi na kuamua hatua iliyo wazi na inayolingana. Wakati huo huo, akaunti za Bw.Trump zimesimamishwa.

Trump alijibu kwa hasira juu ya uamuzi wa jopo la usimamizi akisema

"Uhuru wa kuzungumza umechukuliwa kutoka kwa Rais wa Marekani kwa sababu wenye nguvu wa mrengo wa kushoto walio vichaa wanaogopa ukweli, lakini ukweli utatoka tu kwa nguvu na ukubwa kuliko hapo awali.”

XS
SM
MD
LG