Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:14

Rais Macron awasili Afrika Kusini kwa ziara ya siku mbili


Rais Emmanuel Macron akikagua gwaride la heshima mjini Pretoria, Afrika Kusini.
Rais Emmanuel Macron akikagua gwaride la heshima mjini Pretoria, Afrika Kusini.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa yuko Afrika Kusini kwa ziara ya siku mbili inayozingatia suala la janga la ugonjwa wa Covid 19 na mzozo wa uchumi unaotokana na janga hilo.

Macron aliwasili Afrika Kusini akitokea Rwanda ambako alikiri jukumu la nchi yake kwenye mauaji ya kimbari mwaka 1994, na alizungumza na mwenzake Paul Kagame juu ya kurekebisha tena ushirikiano kati ya nchi zao mbili.

Akiwa Afrika Kusin, taarifa ya ofisi ya rais mjini Pretoria inaeleza kwamba anakutana na mwenyeji wake Cyril Ramaphosa kwa mazungumzo yatakayozingatia juu ya kutengeneza chanjo huko Afrika Kusini na kwengineko barani Afrika na kuondolewa kwa muda haki miliki ya chanjo za COVID-19.

Viongozi hao wawili wanatembelea chuo kikuu cha Pretoria ili kuzindua mpango wa kutengeneza chanjo barani Afrika ambao utapata msaada kutoka Umoja wa Ulaya, Marekani na Benki ya Dunia.

XS
SM
MD
LG