Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 19:32

Kilichowasaidia Rwanda kushinda kwa pointi 78-72 dhidi ya Madagascar


Wachezaji wa timu ya GNBC de Madagáscar.
Wachezaji wa timu ya GNBC de Madagáscar.

Mwenyeji Patriots ya Rwanda imefuzu katika raundi ya pili ya ligi ya mpira wa kikapu ya Afrika kwa kupata ushindi wao wa pili kwa pointi 78-72 dhidi ya GNBC Ya Madagasca katika mchezo uliokuwa na ushindani siku ya Jumatano mjini Kigali.

GBNC walianza kwa Haraka kwa kupata pointi kutoka kwa Kiady Mirojo Razanama-Henina, na kuongoza kwa pointi 14-7 katikati ya robo ya kwanza, lakini pasi kutoka kwa Branson Costner kwenda kwa Prince Ibeh iliwaweka Patriots karibu.

Kujaribu mara mbili kwa Bush Wamokota wa Patriots walifanya mchezo kuwa sare kila time ikiwa na pointi 16.

GNBC iliongoza tena kwa pointi kutoka kwa Alpha Jean Arnol Solondrany baada ya kupata pasi kutoka kwa Kiady Mijoro Razanama-Henina.

Razanama-Henina alikuwa katika mchezo tena kwa kuandikisha pointi, kwa kufunga baada ya kutokea adhabu. Aliendelea kufunga kwa kuruka.

Patriots walirejea tena, na kuongoza kuelekea mwishoni mwa nusu ya kwanza ya mchezo kwa pointi ya Aristide Mugabe.

GBNC ilijibu kwa pointi tatu zilizo fungwa na Razanama-Henna.

Timu ya Madagasca iliongoza tena kwa pointi tatu zilizofungwa na Solondrainy.

Mchezaji wa Patriot Dieudonne Ndizeye alizuia mpira wa Francis Mory aliyekuwa akifunga, na Steve Hagumintwari alifunga baada ya jaribio la kufunga kushindikana la Bush Wamukota.

Hagumintwari alifunga tena baada ya kushinda kufunga pointi tatu, lakini Zico Lucandro aliendelea kuiweka GNBC kwenye mchezo kwa kufunga pointi muhimu.

Patriots waliemdelea kushambulia kupitia kwa Kenneth Gasana, ambaye alimtengenezea Wamukota na kufunga kwa danki kali dakika chache baadaye na wenyeji Patriots kujihakikishia ushindi wa pointi 78-72.

XS
SM
MD
LG