Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 18:50

Ifahamu timu ya Rivers Hoopers ya Nigeria


Timu ya Rivers Hoopers ya Nigeria
Timu ya Rivers Hoopers ya Nigeria

Timu ya Rivers Hoopers ina makao yake Port Harcourt, Nigeria. Ilianzishwa mwaka 2009 kama Royal Hoopers, timu hiyo imeshacheza katika Premier Ligi ya Nigeria tangu kuanzishwa.

Hoopers wameshinda ubingwa wa taifa mara tatu, na kushinda ubingwa mara mbili mfululizo mwaka 2011 na 2012. Ushindi wao wa mwisho ulikuwa mwaka 2019.

Wanafundishwa chini ya usimamizi wa kocha Ogoh Odaudu na usimamizi wa kapteni wao Belema Alamina.

Hoopers walimsajili aliyekuwa beki wa NBA Ben Uzoh, na pia wachezaji wawili wa Marekani Taren Sullivan na Chris Daniels. Walimpoteza nyota wa Nigeria Festus Ezeli kutokana na kuumia.

Siyo mwengine aliyerithi nafasi yake bali ni mchezaji wa kimataifa wa Uganda Robinson Odoch Opong, ambaye timu nyingine za BAL zinamtamani.

Hoopers watachuana na Rwanda Patriots katika mechi ya ufunguzi wa Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Afrika.

XS
SM
MD
LG