Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:42

Ziara ya Macron Rwanda yaelezwa itaimarisha mahusiano


Rais Emmanuel Macron na Rais Paul Kagame wakiwa Ikulu ya Kigali on Mei 27, 2021.
Rais Emmanuel Macron na Rais Paul Kagame wakiwa Ikulu ya Kigali on Mei 27, 2021.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewasili nchini Rwanda Alhamisi kwa ziara yenye lengo la kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili.

Haya yanajiri baada ya miongo mitatu ya mivutano ya kidiplomasia, kuhusu jukumu la Ufaransa katika mauaji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda.

Macron ni kiongozi wa kwanza wa Ufaransa, tangu mwaka 2010, kutembelea taifa hilo la Afrika Mashariki, ambalo kwa muda mrefu limekuwa likiishutumu Ufaransa kwa kuhusika na mauaji ya watu 800,000, wao wakiwa wa jamii ya Watutsi.

Alifika Kigali muda mfupi baada ya saa 7:00 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki, kwa ziara ya siku moja kabla ya kuelekea Afrika Kusini Ijumaa, kulingana na ofisi ya rais wa Ufaransa.

Alitarajiwa kutoa hotuba asubuhi kwenye Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari ya Kigali, ambapo wahanga wengine 250,000 wa mauaji hayo wamezikwa.

Baadhi nchini Rwanda walitarajia ataomba msamaha rasmi kwamba Ufaransa ilishindwa kusaidia kukomesha mauaji kati ya Aprili na Julai 1994.

Rais wa Rwanda Paul Kagame amepuuza umuhimu wa suala hilo, akisema msamaha wowote juu ya jambo hilo ulipaswa kuwa wa hiari.

XS
SM
MD
LG