Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 18, 2024 Local time: 08:50

Ufaransa kuifutia deni la dola bilioni tano nchi ya Sudan


Waziri Mkuu wa Sudan, Abdalla Hamdok
Waziri Mkuu wa Sudan, Abdalla Hamdok

Wakati huo huo Ujerumani pia ilitoa msaada wakati wa mikutano ya kifedha ya hapa na pale ya Paris inayolenga serikali ya mpito ya kidemokrasia ya Khartoum na kurejea kwa hali ya kiuchumi Afrika kutoka janga la virusi vya Corona

Siku mbili za mazungumzo ya ngazi ya juu, karibu na mnara wa Eiffel mjini Paris umewakutanisha zaidi ya darzeni moja ya viongozi wa Afrika, pamoja na wawakilishi wa vyeo vya juu wa taasisi mbali mbali, umoja wa ulaya na China.

Sudan ilikuwa kwenye ajenda ya Jumatatu. Miaka miwili baada ya kumuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu, Omar al-Bashir, nchi hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi, kama wanaharakati wa Sudan Nasreen El Saim alivyoelezea katika hotuba. Ikiwemo mfumuko wa bei kufikia kiwango cha juu cha asilimia 300 na upungufu wa bidhaa za msingi. Sehemu kubwa ya dola zake bilioni 60 katika deni la nje, inadaiwa kwa kile kinachoitwa “wadai wakuu wa klabu ya Paris”.

Emmanuel Macron, Rais wa Ufaransa
Emmanuel Macron, Rais wa Ufaransa

“Napongeza mabadiliko ya mpito ya Sudan kuelekea demokrasia kwamba yanatia moyo, jamii ya kimataifa ilikuwa upande wake, na kwamba nchi hiyo inahitaji kuungwa mkono kiuchumi na kisiasa”.

Waziri Mkuu wa Sudan, Abdalla Hamdok anasema nchi hiyo yenye utajiri wa rasilimali za asili, haitafuti misaada au mchango, lakini badala yake inataka jumuia ya kimataifa iangalie fursa za uwekezaji.

Mazungumzo mapana ya Afrika ya Jumanne yanaangazia kuanguka kwa uchumi kulikotokana na COVID-19, ambayo imesababisha kushuka utalii na sekta nyingine. Mwaka jana bara hilo uchumi wake ulianguka kwa mara ya kwanza, katika zaidi ya miongo mitatu. Benki ya Dunia inakadiria takribani watu maskini milioni 34 wapya wanaishi chini yad ola mbili kwa siku, katika Afrika-kusini mwa jangwa la sahara pekee. Wataalamu wanasema COVID-19 imeliacha bara hilo likikabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha wa bilioni 300.

Mkuu wa IMF, Kristalina Georgieva
Mkuu wa IMF, Kristalina Georgieva

Kabla ya mazungumzo hayo, mkuu wa shirika la fedha Duniani, Kristalina Georgieva, aliiambia France 24 TV, kwamba ana matumaini mataifa Tajiri yatatumia mpango uliopangwa wa kuongeza dola bilioni 650 katika akiba za IMF kusaidia eneo kuwa na nguvu siku za usoni.

“Tunasikia wasi wasi mkubwa kutokana na uchumi tofauti, huku uchumi wa hali ya juu ukijitoa, nchi zenye kipato cha chini ziinajikuta ziko nyuma sana. Kwa nini hii sio wasi wasi wa kimaadili pekee, lakini pia wasi wasi wa kiuchumi. Kwa sababu tofauti hii ingemaanisha ukosefu mkubwa wa usalama, kukosekana kwa utulivu na kupoteza fursa kwa uchumi wa ulimwengu kukua”.

Oxfam International pia ina wasi wasi Afrika iko nyuma, kwa sababu mbali mbali. Peter Kamalingin, mkurugenzi wa program ya Pan Africa ya Oxfam anasema kuipa Afrika nafasi ya ufikiaji chanjo ya COVID-19 pamoja na teknolojia ni muhimu. “Jambo la pili bila shaka ni kwamba tunaona hali nyingi ambapo IMF na Benki ya Dunia zinaendelea kutoa masharti ya mikopo, inajitolea kwa sehemu kubwa hususan kwa sehemu kadhaa zenye watu wasiojiweza”.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi kutoka Rwanda, Msumbiji na Misri, pia unaonekana kama nafasi nyingine kwa Paris kupanua zaidi ushawishi wake kwa nchi zinazozungumza kifaransa barani Afrika.

XS
SM
MD
LG