Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 13:55

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anapanga kuitembelea Rwanda hivi karibuni


Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron

Ninathibitisha nitakwenda Rwanda mwishoni mwa mwezi huu. Hii itakuwa moja ya ziara ya kisiasa na kumbukumbu, lakini pia ya  kiuchumi, alisema Macron mwishoni mwa mkutano wa Africa uliofanyika huko Paris

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema Jumanne kwamba atafanya ziara yake ya kwanza kuelekea Rwanda mwishoni mwa mwezi huu, uwezekano wa kuvunja mivutano katika uhusiano uliofunikwa na jukumu la Ufaransa wakati wa mauaji ya Kimbari mwaka 1994.

Ninathibitisha nitakwenda Rwanda mwishoni mwa mwezi huu. Hii itakuwa moja ya ziara ya kisiasa na kumbukumbu, lakini pia ya kiuchumi, alisema Macron mwishoni mwa mkutano wa Africa uliofanyika huko Paris.

Aliongeza kuwa amekubaliana na mwenzake wa Rwanda, Paul Kagame, ambaye walikutana pembeni ya mkutano wa Jumatatu, kwa ajili ya kuandika ukurasa mpya katika uhusiano.

Ziara yake itakuwa safari ya kwanza kufanywa na Rais wa Ufaransa tangu Nicolas Sarkozy alipoitembelea nchi hiyo mwaka 2010.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame
Rais wa Rwanda, Paul Kagame

Kagame aliwaambia waandishi wa habari kutoka televisheni ya France 24 na Radio RFI hapo Jumatatu kwamba Rwanda na Ufaransa zina msingi mzuri wa kuunda uhusiano baada ya ripoti ya kihistoria, iliyokiri Ufaransa ilikuwa na majukumu makubwa juu ya mauaji ya kimbari yam waka 1994.

Tuko katika mchakato wa kurejesha hali ya kawaida, aliongeza.

Macron aliendelea na kurekebisha uhusiano na Rwanda kwa kuagiza ripoti ya kihistoria katika jukumu la wanajeshi wa Ufaransa kwenye mauaji ya kimbari, ambapo takribani watu laki nane waliuawa.

Ripoti hiyo ilihitimisha mwezi Machi kwamba Ufaransa ilikuwa gizani kwa maandalizi ya mauaji ya watu wengi wa kabila la Watutsi, yaliyofanywa na utawala wa wahutu, ambao waliungwa mkono na Ufaransa.

Kagame katika siku za nyuma ameishutumu Ufaransa kwa kushiriki katika mauaji ya kimbari, lakini akasema alikubali matokeo ya tume ya Ufaransa kwamba Paris haikuhusika katika mauaji hayo.

Sio juu yangu kuhitimisha kuwa hivi ndivyo walipaswa kusema, Kagame alisema. Ni jambo ambalo naweza kulikubali.

XS
SM
MD
LG