Kumekuwepo na madai na malalamiko kwamba Ufaransa chini ya rais Francois Mitterand wakati huo ilikuwa haijawajibika vya kutosha kuzuia mauaji hayo yaliyo sababisha vifo vya karibu watu laki 8 wengi wao Watutsi na hata kutuhumiwa ilishirki kwenye uhalfu huo.
Suala hiilo lingali ni mwiba katika uhusiano kati ya Ufaransa na Rwanda hadi hii leo.
Rais Macron aliamrisha kuundwa kwa tume hiyo ya wanahistora wasio na ujuzi wa masuala ya Rwanda mwezi May mwaka 2019 ili wasiwe na upendeleo kuchunguza jukumu la Ufaransa nchini Rwanda kati ya 1990 hadi 1994 kupita utafiti mbali mbali ulokwisha fanywa.