Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:57

Serikali ya Rwanda yatoa msaada wa chakula kwa watu kutokana na Corona


Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame

Mamlaka nchini Rwanda wameanza kutoa chakula kwa wakaazi katika mji mkuu wa Kigali baada ya shughuli za kawaida kufungwa mjini humo kwa siku 15 kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

Watu wote wanatakiwa kusalia nyumbani isipokuwa wafanyakazi wanaotoa huduma muhimu kama afya na usalama.

Familia 3,000 ambazo zimeorodeshwa kuwa maskini, zimepangiwa kupewa msaada wa chakula.

Mji wa Kigali una karibu watu milioni moja.

Msaada wa chakula unatolewa na wafanyakazi wa msaada ambao wamepimwa na kudhibitishwa kwamba hawajaambukizwa virusi vya Corona.

XS
SM
MD
LG