Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 20:38

EU yaomba mataifa kutoruhusu ndege za Belarus kwenye anga zao


Waandamanaji nchini Poland waitisha kuwachiliwa kwa Protasevich.
Waandamanaji nchini Poland waitisha kuwachiliwa kwa Protasevich.

Umoja wa Ulaya umeyasihi  mataifa wanachama kufunga anga zao pamoja na viwanja vya ndege kwa mashirika ya ndege ya Belarus, baada ya  ndege moja kulazimishwa  kutua kwa dharura mjini Minsk ili kukamatwa kwa mwandishi mmoja wa blogi aliekuwa akikosoa utawala wa kidikteta wa Rais Alexander Lukashenko.

Kufuatia tukio hilo la Jumapili, tayari mashirika kadhaa ya ndege yakiwemo yale ya Ufaransa,Lufthansa na Singapore yamesema kuwa hayatarusha ndege zao kwenye anga ya Belarus.

EU pia inachunguza tukio hilo wakati ikitadhmini kuhusu hatua itakazochukua dhidi ya maafisa wa Belarus waliyo amuru hatua hiyo ichukuliwe.

Tayari kuna maafisa kadhaa kutoka serikali ya Belarus waliowekewa vikwazo na EU kutokana na kuhusika kwenye msako wa mwaka jana baada ya uchaguzi wa rais uliozua utata.

EU pamoja na Marekani wameomba serikali ya Lukashenko kumuachilia mara moja Raman Pratasevich ambaye ni blogger mwenye umri wa miaka 26 na ambaye amekuwa akiishi uhamishoni nchini Poland.

Mtayarishaji - Harrison Kamau

XS
SM
MD
LG